Askofu Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Mtume Dkt. Dunstan Maboya akiambatana na Viongozi wengine wa kanisa hilo wameongoza maombi Maalum ya kumuombea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda na kuwatakia mafanikio mema kwenye kuwatumikia wananchi.

Askofu Dkt. Dunstan Maboya amefika Ofisini kwa Mhe. Paul Makonda, mkuu wa Mkoa wa Arusha akiambatana na Mchungaji Daniel Safari na Nabii Joshua Alamu ambaye ni Rais wa Baraza la Mitume na Manabii nchini Tanzania.

Viongozi hao wa dini Wakiongozwa na Askofu Maboya wameiombea pia mihimili yote ya nchi kwa maana ya Bunge, Mahakama na Serikali na kuwataka kutenda Haki katika kuwatumikia Watanzania.

Aidha Baba Askofu Dunstan Maboya ametumia fursa hiyo kumualika Mhe. Mkuu wa Mkoa kwenye Tamasha kubwa la Muziki wa Injili linalotarajiwa kufanyika Juni 2 mwaka huu Jijini Arusha likitanguliwa na Kongamano la dini linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Paulo Christian Makonda akisalimiana na Mkuu wa Makanisa ya Calvary assemblies of God alipotembelea katika Ofisi hiyo mapema Leo.
Katika picha ni Mtume Dastan Maboya Askofu Mkuu wa Makanila ya Calvary Assemblies of God akiwa pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda wakiwemo viongozi wa dining wengine ambao wametmbelea katika ofisi ya Mkuu huyo wa mkoa mapema Leo

Mkuu wa makanisa ya Calvary Assemblies of God Mtume Dastan Maboya akiongoza Maombi ya kuwaombea viongozi kuanzia ngazi ya zote wa Taifa la Tanzania mapema leo Jijini Arusha
Na Mwandishi wetu, Hanang'

SHIRIKA la Amref Tanzania na shirika la Marekani la kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) limewanufaisha wanafunzi 3,000 wa shule za msingi na sekondari wilaya ya Hanang' mkoani Manyara, baada ya kuwajengea miundombinu ya kudhibiti magonjwa ya milipuko.

Mashirika hayo yamewanufaisha wanafunzi hao kwa kuzindua maeneo ya kunawa mikono na kukarabati vyoo.

Mkurugenzi mkazi wa Amref Tanzania, Dkt Florence Temu amesisiza umuhimu wa mbinu jumuishi za kuimarisha magonjwa ya mlipuko katika jamii kupitia ufuatliaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira.

Amesema maendeleo makubwa yaliyopatikana katika ufuatiliiaji wa mapema na kukabiliana na vitisho vya afya ya umma katia kanda hiyo hasa magonjwa ya mlipuko,

Dkt Temu amesema ushirikiano kati ya Amref Tanzania na Kituo cha serikali ya Marekani (CDC) Tanzania, umekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ushauri na uhamasishaji katika uboreshaji wa huduma za maji na usafiwa mazingira hivyo kusababisha kuzuia magonjwa ya kuambukiza katika kanda.

Mkuu wa usalama na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira Wizara ya Afya, Dkt Honestus Anicetus ameipongeza serikali ya Tanzania, kituo cha serikali ya Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) Tanzania na Amref Tanzania kwa juhudi zao za kuunga mkono serikali kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa mazingira.

Dkt Anicetus amesema serikali imeboresha Sekta ya afya kupitia miradi mbalimbali ya afya nchini kwa uwajibikaji wa utunzaji wa maeneo hayo na

Amesisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwa yeyote atakayesababisha uharibifu au uzembe.

Mkurugenzi wa Kitengo cha ulinzi wa afya, katika kituo cha serikali ya Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) Tanzania, Dk Wangeci Gatei amesema dhamira ya CDC Tanzania kuimarisha mbinu za kuzuia maambukizi ya magonjwa ya mlipuko Tanzania kupitia juhudi za ushirikiano na serikali na washirika wa ndani.

Amesema lengo ni kuisaidia Tanzania katika kuzingatia kanuni za kimataifa za afya (2005) kupitia malengo ya Global Health Security Agenda (GHSA) 2024.

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Ganana, Emmanuel Amani amesema wanashukuru kwa msaada huo utakaowanufaisha wao.

Ofisa afya wa mkoa wa Manyara, Sultan Mwabulambo amepongeza hatua hiyo kwani umuhimu wake ni mkubwa kwa wanafunzi wa maeneo hayo ambayo yalikumbwa na maafa mwishoni mwa mwaka jana.

Mwakilishi wa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hanang' Dk Mohamed Kodi amesema miundombinu hiyo itakuwa kichocheo kikubwa kwa wanafunzi hao kupata elimu kwenye mazingira rafiki.

Hafla ya makabidhiano hayo imehudhuriwa na mwakilishi wa Wizara ya Afya, kituo cha Serikali ya Marekani (CDC) Tanzania, Amref Tanzania na viongozi wa Serikali za mitaa, wahudumu wa afya ya jamii, walimu na wanafunzi.


Katika kuendeleza ushirikiano na wateja wake, Exim Bank imeingia makubaliano na Mgahawa wa Chef’s Pride ikiwa ni pamoja na kutoa punguzo na ofa mbalimbali kwa wateja wake watakaotumia kadi za benki hiyo kufanya miamala ya malipo. Tukio hili pia liliambatana na uzinduzi rasmi wa mgahawa wa Chef’s Pride uliofanyika jijini Dodoma.

Hafla hiyo iliyoudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule kama Mgeni Rasmi, ilifanyika jijini Dodoma ambapo Mhe. Rosemary aliwapongeza Exim Bank mashirikiano hayo.

“Serikali tunawapongeza benki ya Exim kwa maamuzi yao ya kuja kuwekeza Dodoma kama sehemu ya kusogeza huduma kwa wateja wao popote pale walipo. Tunahimiza na kuwakaribisha wawekezaji wengine kuiga mfano huu wa Exim Bank,” alisema Mhe. Rosemary.

Akizungumzia mashirikiano hayo, Meneja Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Wa Exim Bank, Bi. Kauthar D’souza alisema, “Benki ya Exim tumekuwa na kawaida ya kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora za kifedha kwendana na mabadiliko ya kidijitali yanayotokana na maendeleo ya teknolojia. Tunafuraha kubwa kuungana leo na mgahawa wa Chef’s Pride katika kuboresha huduma zetu kwa wateja hasa matumizi ya kadi za benki yetu.”

Ushirikiano huu pia unalenga kukuza urahisi na usalama wa miamala ya wateja wa benki hiyo. Halikadhalika, ushirikiano huu ni mwendelezo wa jitihada za benki ya Exim kuongeza matumizi ya kufanya miamala kupitia kadi zao ili kuwapa fursa wateja wake kufurahia ofa mbalimbali pamoja na punguzo. Pia, kwa yule ambaye hana akaunti na Exim Bank anaweza kutembelea tawi lolote la Exim na kupata kadi yake ya malipo ya kabla (Prepaid) ili kuweza kufurahia ofa hii.

Kupitia huduma hii, mteja ataweza kutumia kadi yake kufanya miamala ya malipo na kupata punguzo maalumu na ofa zingine utakapofanya miamala ya malipo kwa kutumia kadi yetu.

Akielezea baadhi ya ofa hizo, Kauthar alisema, “Wateja watakaowahi kupata kadi za Exim bank na wale watakaotumia fedha zaidi wataondoka na zawadi za vocha na kadi za malipo ya kabla yenye fedha ndani yake.”

Exim Bank imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini katika sekta kadhaa kama vile uchumi, uwezeshaji, elimu, afya, mazingira, usalama, na teknologia kupitia sekta binafsi pamoja na serikali ya Tanzania.

Mkuu wa Idara ya Huduma za Kadi na  Malipo wa Exim Bank, Paritosh Babla (kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgahawa wa Chef's Pride, Salim Mahsen Al Amry, wakisaini makubaliano ya ushirikiano katika uzinduzi rasmi wa tawi la Chef's Pride Dodoma. Kupitia ushirikiano huu, wateja wa Benki ya Exim watapokea ofa mbalimbali na punguzo wanapofanya malipo kwa kutumia kadi zao za Exim Bank. Tukio lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary S. Senyamule, kama Mgeni Rasmi.












WIZARA ya Uchukuzi kupitia Shirka la Reli Tanzania – TRC limefanya semina elekezi kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR unaoendelea, semina imefanyika katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, Mei 2023.

Lengo la Semina ni kuwajengea uelewa wa pamoja wabunge kuhusu mradi wa ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa unaoendelea awamu ya kwanza Dar es Salaam – Mwanza, awamu ya pili Tabora – Kigoma pamoja na vipande va Mtwara – Mbambabay na Uvinza – Msongati.

Semina iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Mhe. Moshi Selemani Kakoso ambapo Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania – TRC walitoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali na kujibu maswali ya wabunge.

Mhe. Kakoso amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya kutenga fedha zaidi ya Trilioni 10 kutekeleza mradi pia amempongeza Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa kuhakiksha miradi inakamilika kupitia jitihada za kuhakikisha Fedha kwaajili ya mradi zinapatikana.

“Mliowapa dhamana (Shirika la Reli) wamefanya kazi kubwa kwenye usimamizi na lipo jambo kubwa limefanywa na menejimenti ya TRC wabunge hamlifahamu, kwenye mikataba walioingia na wakandarasi suala la gharama wamelizingatia kiasi kwamba hata mradi ukiongezeka gharama mkataba utabaki vilevile” aliongeza Mhe. Kakoso

Aidha, akifunga Semina Mhe. Kakoso ameiomba Serikali ikamilishe hatua za kupata wawekezaji kwaajili ya kuanza mradi wa reli ya Mtwara kwenda Mbamba bay kupitia Liganga na Mchuchuma, ameiomba Serikali iweke mkakati wa kuhakikisha miundombinu iliyojengwa kwa gharama kubwa inalindwa pia Serikali ihakikishe wakandarasi wadogo wanaofanya kazi kwenye mradi wanalipwa pamoja na kuwekeza kwenye rasilimali watu

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Makame Mbarawa ametolea ufafanuzi kuhusu suala la nauli za treni ya mwendokasi kuwa TRC haina mamlaka ya kutangaza nauli isipokuwa ni suala la kisheria hivyo Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini – LATRA inaendelea na mchakato na nauli ziatatangazwa ambapo kila mwananchi ataweza kumudu gharama za kusafiri na treni ya mwendokasi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa alitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa SGR pamoja na maandalizi ya kuanza utoaji huduma mapema mwezi Julai 2024. Kadogosa alieleza hatua iliyofikiwa kwaajili ya kuanza ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa kutoka Mtwara hadi Mbamba bay na Uvinza Msongati.

Bunge la bajeti kwaajili ya mwaka 2024/25 linaendelea ambapo Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi inatarajia kusomwa Bungeni tarehe 6 Mei 2024 jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya uwasilishwaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 huku mradi wa SGR ukichukua kiasi kikubwa cha bajeti ya Wizara na Serikali kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea katika sekta ya reli nchini.

-Wawatuhumu kuogopa kuulizwa uuzaji wa ardhi

Na Mwandishi wetu, Simanjiro 

WAKAZI wa Kijiji cha Loiborsiret Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamewashukia Mwenyekiti wa kijiji hicho  Kimaai Saruni na Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Aloyce Teme kwa kukacha mkutano wa Diwani wa kata ya Loiborsiret, Ezekiel Lesenga (Maridadi).

Wananchi hao wamedai kuwa viongozi hao wamegoma kushiriki mkutano wa Diwani wao wa kusoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kuhofia kuulizwa maswali magumu juu ya uuzwaji wa ardhi ya kijiji hicho.

Mmoja kati ya wakazi hao Lazaro Lambagi amesema hofu ya kuulizwa maswali magumu kutokana na kuuza ardhi kumesababisha viongozi hao kutohudhuria mkutano huo.

"Aliyekuwa DC Simanjiro Dkt Suleiman Serera aliagiza viongozi kusimamisha uuzaji ardhi hadi uchaguzi wa serikali za mitaa upite ila hawa wao wameendelea kuuza kwa kificho na kuogopa mikutano," amesema.

Mkazi mwingine Kalai Mollel amesema viongozi hao wameshiriki kuuza eneo la ardhi ya kitongoji cha Oltepelek kwa kuong'oa vibao vya eneo la malisho na kuviweka ofisi ya kijiji cha Loiborsiret.

" Tumelalamikia suala hili la uuzwaji ardhi kwa muda mrefu ila viongozi hawa wamekuwa wabishi ila mwisho wao umefika kwani wauza ardhi wote tumewabaini,"  amesema Mollel.

Kwa upande wake Leronjo Lembaji amesema amesikitishwa na viongozi hao kususia mkutano wa Diwani anayetokana na CCM.

Naye, Mwenyekiti wa kijiji cha Loiborsiret, Kimaai Saruni amesema hakuwa na taarifa ya kufanyika kwa mkutano huo wa Diwani ndiyo sababu hakuweza kuhudhuria.

Kimai hakuwa tayari kuzungumza juu ya tuhuma za yeye kuuza ardhi akieleza kuwa atazungumza suala hilo siku nyingine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM kata ya Loiborsiret, Aloyce Teme amesema hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kutokuwa na taarifa.

"Suala la kuuza ardhi ya kijiji anayetakwa kuulizwa ni Mwenyekiti wa kijiji ila nilishindwa kufika kwenye mkutano kwa sababu sikualikwa," amesema Teme.

Afisa mtendaji wa kata hiyo, Mary Chisoji amesema taarifa za kuwepo kwa mkutano huo zilishatolewa kwa barua kwa viongozi wote wa eneo hilo.

Chisoji amesema kuhusu suala la uuzwaji ardhi holela wenyeviti wote walishapewa onyo la kutouza ardhi hadi uchaguzi wa serikali za mitaa utakapofanyika.

"Hili la kurejeshwa kwa vibao viling'olewa vya malisho kitongoji cha Oltepelek tutavirejesha baada ya wiki moja wananchi msijali kuhusu hilo," amesema Chisoji.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho Upendo Menaki Sawaki ambaye ameshiriki mkutano huo amesema viongozi wote walipewa taarifa ya kuwepo mkutano huo hivyo kitendo cha kudai kuwa hawana taarifa siyo sahihi.

Hata hivyo, Diwani wa Kata hiyo Ezekiel Lesenga Maridadi amesema kitendo cha viongozi hao kususia ziara yake kimemkwaza na kumsikitisha kwani kimeonyesha ni siasa chafu.

"Nimekuja kuelezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kupitia mikutano ili tuone mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan na kusikiliza kero na changamoto za watu ila viongozi hao hawakufika," amesema.

Amesema suala la kung'olewa vibao vya eneo la malisho atalisimamia ipasavyo kwani yeye hakuwepo wakipanga matumizi bora ya ardhi kupitia mkutano wa kijiji chao.

"Kwa sababu mliamua wenyewe eneo hilo liwe la malisho nitaweka miguu yangu hapo kutetea hilo na kama viongozi hao wameshiriki kuuza watakuwa wamejiharibia," amesema Maridadi.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amewaagiza wataalamu wa serikali kushirikiana na taasisi binafsi zinazotekeleza miradi mkoani humo kutekeleza miradi yao kwa ufanisi na kupata matokeo chanya kutokana na fedha nyingi wanazotumia kwenye utekelezaji wa miradi hiyo.

Mtaka ametoa maagizo hayo wilayani Wanging'ombe baada ya kushindwa kuridhishwa na kazi anayoifanya afisa kilimo wa kata ya Igwachanya Benny Mgaya anayehudumia vijijiji vya Chalowe na Mtapa kutokana na kufeli kusimamia mradi wa mboga mboga uliopo kwenye shule ya msingi Chalowe uliosaidiwa na shirika la Care International wanaotekeleza mradi wa SADIFU kwa kulima mashamba 57 ya mfano kwa mazao tofauti ikiwemo zao la Soya na mashamba 27 ya mboga mboga mashuleni.

"Kwa hiyo ni lazima maafisa kilimo wahakikishe maeneo yote ambayo care wasaidia miradi ya mboga mboga,idara ya kilimo wawajibike na wawe wanafuatilia mara kwa mara kwasababu hili sio shamba ambalo linafanana na mtu wa kilimo kusimamia,mimi nilijua ni wanafunzi wenyewe wanajilimia yani mtu wa kilimo yupo shamba linakuwa na kifadulo hivyo"amesema Mtaka

Aidha Mtaka amepongeza shirika hilo kwa kufanya vizuri kwenye mashamba darasa ya soya na kuwaomba kuongeza nguvu kwenye miradi ya mboga mboga mashuleni ili watoto waweze kupata mboga kutokomeza udumavu pamoja na kuongeza ukubwa wa mashamba darasa.

"Sasa piaga picha unakuwa na eka kumi shamba lipo hivi na ni haki hawa wanaopita na magari wanasimama na kupiga picha hili shamba ni zuri unawez ukapiga picha na kupeleka kokote duniani"aliongeza kusema Mtaka alipokagua shamba la mfano la Soya lililopo kijiji cha Matowo

Kwa upande wake afisa kilimo wa kata hiyo Benny Mgaya ameeleza sababu ya shamba hilo kuharibika

"Mh,eneo hili lilikuwa linatumika kama bustani miaka ya nyuma kwa samadi ilikuwa inamwagwa lakini kwa mwaka huu hatujamwaga lakini pia tumekuwa na changamoto ya maji"amesema Benny

Lilian Mkusa ni meneja wa mradi huo amesema shirika limepokea changamoto hizo huku akiongeza kuwa kutokana na mahusiano waliyonayo na taasisi ya utafiti wa kilimo Tari Uyole wanakwenda kusaidia mbegu wakulima katika msimu ujao wa kilimo.

"Msimu ujao wa kilimo tutasaidia wakulima kupata mbegu kutoka TARI Uyole na kuzileta hapa hapa bila mkulima kutumia nauli yeyote kuzifuata mbegu na sisi tumeoka kuja kwako imekuwa ni kitu kikubwa sana"amesema Lilian

Nao baadhi ya viongozi wa Chama na serikali wilaya ya Wanging'ombe akiwemo mkuu wa wilaya hiyo Claudia Kitta wamesema wako tayari kwenda kusimamia maelekezo ya mkoa juu ya miradi inayotekelezwa wilayani humo.




 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo wa pili kutoka kushoto akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Kituo Maalumu za kurahisisha huduma za Uwekezaji Nchini, Kutoka Kulia ni Meneja Uhusiano wa Azania Bank, Halima Semhunge, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jarida la taarifa za mafanikio ya mwaka mmoja wa TIC, Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida na kulia ni Kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri.
Kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida,   na Meneja Uhusiano wa Azania Bank, Halima Semhunge wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionesha jarida baada ya kuzinduliwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo  akizungumza mara baada ya kudindua jarida la taarifa za mafanikio ya Mwaka mmoja wa TIC.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida  wa pili kutoka kushoto akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha Maalumu kwaajili ya kurahisisha huduma za uwekezaji nchini. Kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo na Meneja Uhusiano wa Azania Bank, Halima Semhunge.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Maalumu cha kuhudumia wawekezaji kitacho wawezesha kupata huduma kwa haraka zaidi pamoja na baahi ya wawekezaji.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, amezindua kituo maalumu cha kuhudumia wawekezaji kitacho wawezesha kupata huduma kwa haraka zaidi

Kituo hicho kilichozinduliwa leo Mei 04, 2024 kimejengwa na benki ya Azania kwa lengo la kuokoa muda wa wawekezaji wanaokuja nchini kwaajili ya uwekezaji.

Akizungumza mara baada ya kuzindua kituo hicho jijini Dar es Salaam, Profesa Mkumbo, amesema kituo hicho ni maalumu kwa  kuhudumia wawekezaji  katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kusaidia wawekezaji wanaokuja nchini kusajili kampuni kwa haraka zaidi ambapo  zoezi la kusajili lilikuwa likichukua muda mrefu.

"Tumeamuwa kufungua kituo hiki ili  Mwekezaji akija aweze kusajili kampuni yake hapa na anapotoka awe na cheti cha usajili wa kampuni yake.“ Amesema.

Amesema katika kituo hicho watakuwepo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) pamoja na wanasheria ambao watasaidia wawekezaji kusajili kampuni zao kwa kuzingatia sheria za Tanzania.

Kwa mujibu wa Prof. Mkumbo amesema kituo hicho kitasaidia kuvutia wawekezaji wengi kutoka nje na ndani ya nchi hivyo wawekezaji hao watatoa fursa za ajira kwa wananchi pamoja na uchumi wanchi kukua.

Aidha amesema kuwa wataendelea kutekeleza maoni ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuvutia wawekezaji wengi zaidi kwa kupitia TIC na kituo hicho kilichojengwa na Benki ya Azania.

“Tupo katika ushindani na kuvutia wawekezaji kutoka duniani na moja ya eneo ambalo wanaangalia ni uharaka wa kuhudumiwa maana yake kwa kufungua kituo cha kusajili kampuni hapa hapa inamanisha kwamba Mwekezaji atapo kuja Tanzania atahudumiwa haraka iwezekavyo na kuaanza shughuli zake mapema.” Ameongeza

Pia ameeleza kuwa Wawekezaji wote wa ndani na nje watahudumiwa kwa usawa na Mwekezaji atakaye ingiza mtaji mkubwa Tanzania atapata huduma maalum.

Kwa Upande wa Meneja Uhusiano wa Azania Bank, Halima Semhunge, amesema kuwa hiyo ni sehemu moja tuu ya utekelezaji wa maeneo ambayo wanaenda kishirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania pia ni kwaajili ya kuunga mkono juhudi za kituo hicho katika kuongeza Wawekezaji Nchini.

"Kipekee tunafuraha sana kushiriki katika uzinduzi wa Kituo hiki kwaajili ya kurahisisha na kuahamasisha uwekezaji nchini na nje ya nchi.

Amesema Mwekezaji atakapofika katika kituo hicho atakutana na huduma zote na kupata huduma za kifedha pamoja na Kufungua akaunti kupitia Benki ya Azania.

Na Mwandishi wetu, Hanang'

SHIRIKA la Amref Tanzania na shirika la Marekani la kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) limewanufaisha wanafunzi 3,000 wa shule za msingi na sekondari wilaya ya Hanang' mkoani Manyara, baada ya kuwajengea miundombinu ya kudhibiti magonjwa ya milipuko.

Mashirika hayo yamewanufaisha wanafunzi hao kwa kuzindua maeneo ya kunawa mikono na kukarabati vyoo.

Mkurugenzi mkazi wa Amref Tanzania, Dkt Florence Temu amesisiza umuhimu wa mbinu jumuishi za kuimarisha magonjwa ya mlipuko katika jamii kupitia
ufuatliaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira.

Amesema maendeleo makubwa yaliyopatikana katika ufuatiliiaji wa
mapema na kukabiliana na vitisho vya afya ya umma katia kanda hiyo hasa magonjwa ya mlipuko,

Dkt Temu amesema ushirikiano kati ya Amref Tanzania na Kituo cha serikali ya Marekani (CDC) Tanzania, umekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ushauri na uhamasishaji katika uboreshaji wa huduma za maji na usafiwa mazingira hivyo kusababisha kuzuia magonjwa ya kuambukiza katika kanda.

Mkuu wa usalama na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira Wizara ya
Afya, Dkt Honestus Anicetus ameipongeza serikali ya Tanzania, kituo cha serikali ya Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) Tanzania na Amref Tanzania kwa juhudi zao za
kuunga mkono serikali kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa mazingira.

Dkt Anicetus amesema serikali imeboresha
Sekta ya afya kupitia miradi mbalimbali ya afya nchini kwa uwajibikaji wa utunzaji wa maeneo hayo na

Amesisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwa yeyote atakayesababisha
uharibifu au uzembe

Mkurugenzi wa Kitengo cha ulinzi wa afya, katika kituo cha serikali ya Marekani cha kudhibitina kuzuia magonjwa (CDC) Tanzania, Dk Wangeci Gatei amesema dhamira ya CDC Tanzania kuimarisha mbinu za kuzuia maambukizi ya magonjwa ya mlipuko Tanzania kupitia juhudi za ushirikiano na serikali na washirika wa ndani.

Amesema lengo ni kuisaidia Tanzania katika kuzingatia kanuni za kimataifa za afya (2005) kupitia malengo ya Global Health Security Agenda (GHSA) 2024.

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Ganana, Emmanuel Amani amesema wanashukuru kwa msaada huo utakaowanufaisha wao.

Ofisa afya wa mkoa wa Manyara, Sultan Mwabulambo amepongeza hatua hiyo kwani umuhimu wake ni mkubwa kwa wanafunzi wa maeneo hayo ambayo yalikumbwa na maafa mwishoni mwa mwaka jana.

Mwakilishi wa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hanang' Dk Mohamed Kodi amesema miundombinu hiyo itakuwa kichocheo kikubwa kwa wanafunzi hao kupata elimu kwenye mazingira rafiki.

Hafla ya makabidhiano hayo imehudhuriwa na mwakilishi wa Wizara ya Afya, kituo cha Serikali ya Marekani (CDC) Tanzania, Amref Tanzania na viongozi wa Serikali za mitaa, wahudumu wa afya ya jamii, walimu na wanafunzi.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa leo tarehe 03 Mei 2024 amewaongoza Watumishi wa Wizara kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayoweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi.

Akizungumza alipowasili Mamlaka ya Ngorongoro, Balozi Mussa amesema Wafanyakazi hao waliokuwa jijini Arusha kushiriki Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika tarehe 02 Mei 2024, wametumia fursa hiyo kutembelea na kujionea kwa macho eneo hilo ambalo ni la kipekee duniani ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania kupitia njia mbalimbali ikiwemo filamu ya Tanzania: The Royal Tour.

Kadhalika, amesema Wizara kama mdau wa sekta ya utalii nchini imetumia mkutano wa Baraza Kama fursa kwa kuwapa Wafanyakazi nafasi ya kufanya utalii wa ndani, ili kujifunza na kujenga uwezo wa kutangaza kivutio hicho na vingine vingi kikamilifu kutokana na kujionea kwa macho na kupata kwa undani taarifa muhimu kuhusu vivutio hivyo.

"Si vyema unapomwambia mtu kuhusu kitu fulani wakati wewe mwenyewe hukijui au hujafika, kwani tunaamini kwamba kuona ni kuamini. Hivyo tupo hapa kujifunza na kuwafunza wengine kuhusu utalii wa ndani na tusiwaambie tu wageni kuhusu eneo hili wakati sisi wenyewe hatulijui" amesema Balozi Mussa.

Kadhalika amepongeza jitihada za Mhe. Rais Dkt Samia za kutangaza utalii hususan kupitia filamu ya The Royal Tour na kusema matunda yake yameonekana kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii kutoka ndani na nje ya nchi wanaotembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

"Filamu ya Royal Tour iliyoongozwa na Mhe. Rais Samia haikutoa matokeo kwa watu wa nje tu bali imetoa matokeo, mvuto na ushawishi hata kwa wananchi wa ndani wakiwemo Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki tunaunga mkono na tunatekeleza kile ambacho Mhe. Rais amekianza na kimeleta ushawishi mkubwa kwa watu kutembelea nchini", amesema Balozi Mussa.


Balozi Mussa ametumia wasaa huo kutoa wito kwa wananchi wa Tanzania na wageni kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kujionea wanyama wakubwa watano maarufu kama "The Big Five" wanaopatikana katika Hifadhi hiyo kama Simba, Tembo, Chui, Nyati na Faru.


Kwa upande wake, Afisa Utalii wa Mamlaka ya Ngorongoro, Bw. Orgoo Mauyai amesema Ngorongoro ni ya kipeee na tofauti na hifadhi nyingine duniani kutokana na binadamu na wanyamapori kuishi pamoja na Mamlaka hiyo ni urithi wa dunia chini ya Shirika la Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameipongeza Wizara kwa kuitembelea Mamlaka hiyo.

Pia amewahimiza Wafanyakazi wa Wizara hiyo na Watanzania kwa ujumla kuendelea kupiga kura ili Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro itetee ushindi wake wa nafasi ya kwanza ya kuwa Kituo Kinachoongoza Kuvutia Watalii Afrika iliyoupata mwaka 2023 kwa kupiga kura kupitia Tovuti ya utalii ya www.worldtravelawards.com. Ili kuwa mshindi wa kipengele hicho kwa mwaka 2024.

Nao Wafanyakazi wa Wizara waliopata fursa ya kushiriki ziara hiyo wameupongeza Uongozi wa Wizara hiyo kwa kuwawezesha kutembelea hifadhi hiyo kwani imewawezesha kufahamu mambo mengi yenye manufaa katika utekelezaji wa majukumu yao na katika maisha yao kwa ujumla.

"Nimefurahi kuwa hapa leo. Nimejionea kwa macho uzuri wa hifadhi hii napongeza viongozi waliofanikisha hili kwani tumejifunza mengi" alisema Bi. Lilian Mushi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo amewaongoza Wafanyakazi wa Wizara leo tarehe 03 Mei 2024 kutembelea Mamlaka hiyo ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayoweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi. Wafanyakazi hao waliokuwa jijini Arusha kushiriki Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika tarehe 02 Mei 2024, walitumia fursa hiyo kutembelea na kujionea kwa macho eneo hilo la kipekee duniani

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki, Bi. Chiku Kiguhe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Anayesuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa

Afisa Maliasili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bw. Orgoo Mauyai akitoa ufafanuzi kuhusu Hifadhi hiyo ambayo aliielezea kama ya kipekee kwa vile ni makazi kwa binadamu na wanyama

Balozi Mussa na Wafanyakazi wa Wizara wakimsikiliza Afisa Maliasili Bw. Mauyai akitoa ufafanuzi kuhusu Mamalaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Maelezo yakiendelea


Wafanyakazi wakisikiliza maelezo kuhusu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro


Sehemu nyingine ya Wafanayakzi wa Wizara


Wafanayakazi wa Wizara wakisikiliza maelezo kuhusu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Sehemu nyingine ya Wafanyakazi wa Wizara



Maelezo yakitolewa

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa (wa pili kushoto) akiwa pamoja na wenyeji wake alipowasili katika geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Kushoto ni Afisa Maliasili, Bw. Orgoo Mauyai na Wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara mara baada ya kuwasili katika geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kujionea kivutio hicho cha utalii ili kuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza ndani na nje ya Tanzania



Wafanyakazi wa Wizara wakipata picha kufurahia ziara hiyo



Wafanyakazi wa Wizara katika picha



Msafara wa Magari ya Utalii yaliyobeba wafanyakazi wa Wizara kuelekea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Wizara na Wafanyakazi walipowasili kwenye sehemu maalum ya kuonesha bonde la Ngorongoro



Picha ya pamoja









Wafanyakazi wa Wizara wakipata picha za bonde la Ngorongoro linaloonekana kwa mbali





Picha ya pamoja




Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mussa akiangalia wanyama mbalimbali baada ya kuwasili katika bonde la Ngorongoro. Anayechukua tukio ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Chiku Kiguhe





Ziara katika bonde la Ngorongoro ikiendelea






Tembo ambaye ni mmoja wa wanyama mashuhuri watano wanaojulikana kama The Big Five akiwa Ngorongoro




Viboko nao wanapatikana Ngorongoro




Pundamilia




Tembo




Simba ambaye ni mmoja wa wanyama mashuhuri watano wanaojulikana kama The Big Five akiwa Ngorongoro






Ziara ikiendelea katika bonde la Ngorongoro

















Top News